Kutiana Hasara π
Nilivyowaona nikataka kula chocho kumbe demu aliniona akaniita na kuniuliza "Oooh. Zephiline unafanya nini hapa?" kutokuonesha unyonge nikamjibu "Mke wangu kajifungua kwahiyo nimekuja dukani kuja kununua vitu vya Mtoto" yote ili kumtambia aumie
Nimeingia dukani wote wawili wakawa wananikodelea mimacho ili wajue nitanunua nini
Basi nikanunua nguo za mtoto aina tofauti tofauti
Nikanunua Boksi la pafyum, taulo, viatu, beseni, sabuni halafu nikanunua na poda
Nikalipa kitu kama LAKI MBILI hivi na nilipotoka nikaita Tax nikapanda na kuwaacha wakinikodolea macho kwa Wivuπ
Sasa ombi langu kwenu kama kuna mtu mwenye mtoto mdogo nauza nguo kwa bei nafuu hata elfu 50 ilimladi nipate japo nusu ya hela yangu maana toka asubuhi nahanhangaika mimi kuzitembeza hizi nguo bila mafanikio
Wale washenzi wamejua kunitia hasara leo basi tuπ° #ChekanaZephiline
Chapisha Maoni