Ulikufa Kijinga π
Mzimu Zephiline: Duh, mwenzangu ulikufa vipi?
Mzimu James: Nilifungiwa kwenye friji nikateseka sana hadi nikafa kwa kukosa hewa
Mzimu Zephiline: Duh! pole sana na ulikufa kifo kibaya sana
Mzimu James: Mwenzangu ulikufaje?
Mzimu Zephiline: Nilikufa kwa presha maana nilisikia mke wangu ana kidume ndani nikaenda mbio kuwafumania lakini nilipofika nikakagua kila sehemu sikuona hicho kidume ingawa nilikuwa nina uhakika kabisa kipo mle ndani, basi presha ikapanda nikaanguka na kufariki
Mzimu James: Wewe ndio ulikufa kifo cha kijinga sana maana ungeangalia kwenye friji wote tungekuwa hai sasa hivi
π€£π #ChekanaZephiline
Chapisha Maoni