Siri Kubwa 😲

KIJANA mmoja mtanashati aliingia kwenye hoteli moja kama mteja akaomba aonane na bosina baada ya kuruhusiwa mazungumzo yalikuwa hivi:

Mteja: Samahani, naomba kujua kama chumba namba 39 kiko wazi
Bosi: Ndiyo kiko wazi
Mteja: Naweza kukipata hicho chumba?
Bosi: Ndiyo unaweza kupata
Mteja: Ahsante sana

Baada ya mazungumzo hayo kijana alilipia chumba alichohitaji
Kabla ya kwenda chumbani mteja alimuomba bosi amletee Kisu cheusi, Uzi mweupe wenye urefu wa sentimita 39 na Machungwa 39
Bosi alikubali japo alishangazwa sana na vitu alivyoagizwa na mteja wake
Baada ya hapo mteja alikwenda chumbani bila kuagiza chakula wala kitu kingine chochote

Kwa bahati chumba cha bosi kilikuwa jirani na cha mteja huyo
Usiku wa manane, bosi alisikia sauti za ajabu na kuogofya
Sauti kama za wanyama mwitu wakishambuliana pamoja na sauti za vyombo vikivunjwa sakafuni
Siku hiyo bosi hakupata hata tone usingizi yaani hakulala kabisa kwani alibaki akistaajabu na kutafakari sababu za sauti zile

Asubuhi ya siku iliyofuata wakati mteja akikabidhi funguo za chumba kwa ajili ya kuondoka zake bosi akaona hapana huyu si wa kumwacha
Akamtaka wafuatane hadi chumbani kuhakiki usalama

Walikwenda pamoja hadi chumbani na kukuta kila kitu kikiwa sawa bin sawia zaidi alikutana kile Kisu cheusi, Uzi mweupe na Machungwa vikiwa juu ya meza
Bosi alibaki mwenye huzuni na taharuki asijue siri ya mkasa ule

Mwaka mmoja baadaye mteja yule aliibuka tena hapo hotelini akaomba tena kuonana na bosi
Bosi alihamanika vilivyo kumuona mteja wake wa siku nyingi utadhani ameona jini

Kama awali mahitaji ya mteja yalikuwa yale yale
Chumba namba 39
Kisu cheusi
Uzi mweupe sentimita 39 na machungwa 39

Safari hii bosi alijiapiza kuutafuta ukweli kwa njia yoyote ile
Alimkirimu mgeni wake kama ilivyo ada kisha usiku alibaki macho kusubiri sauti zile za ajabu

Usiku wa manane balaa likaanza
Sauti za ajabu ajabu na ghasia vilianza na safari hii kwa sauti ya juu maradufu ya ile ya mwaka mmoja nyuma

Asubuhi kulipopambazuka mteja aliondoka akiwa na furaha na bashasha na chumba kilikuwa salama u salimini
Bosi alihamaki baada ya kushindwa kubaini siri iliyogubikwa na mkasa ule alibaki anajiuliza
Kwanini chumba namba 39?
Kwanini machungwa tisa?
Kwanini kisu cheusi?
Kwanini uzi mweupe?
Basi kwa kukosa majibu ya maswali hayo bosi aliomba uzima tu kwa Mungu wake ili mwaka utakaofuata mteja huyo afike tena hotelini hapo

Kama mzaha vile mwaka uliofuata mteja yule alirejea na mahitaji yale yale kama ya miaka miwili iliyopita
Kama kawaida usiku Bosi alitaabishwa na hali ile ile ya sauti za kelele na za kutisha

Ilipofika asubuhi wakati mteja akiondoka Bosi alimtaka radhi na kumuomba amweleze siri iliyo nyuma ya yote yaendeleayo chumbani kila afikapo hotelini hapo

Mteja: Ni siri kubwa mno. Je, nikikwambia utaweza kuitunza na kuidhibiti bila kuivujisha?
Bosi: Nakuahidi sitaivujisha siri hiyo, nijulishe!

Bahati iliyo mbaya kwangu na kwako mpaka hivi sasa niandikavyo habari hizi Bosi hajavujisha siri aliyosimuliwa
Tuombe uzima siku akiivujisha siri akanisimulia tu nami nitaiandika hapa kwa ajili yenu😂 #ChekanaZephiline
See Also :