Tupunguzeni Ujuaji π
Kufika nyumbani kwa furaha waliyopata wazazi Mama aliamua kurosti kuku wawili kwa ajili yao
Mezani Zephiline akataka kuwadhihirishia kuwa yeye ni msomi akawaambia wazazi "Hawa Kuku unaona wako wawili ila kwa kutumia sheria za Arthematic na Geometric kuna Kuku watatu mezani"
Mama "Hee! Hebu tuoneshe mwanangu"
Zephiline akachukua Kuku wa kwanza akainua juu akauliza "Ngapi?" wazazi wakajibu "Moja" akainua wa pili akauliza "Ngapi?" wazazi tena kwa umakini mkubwa wakajibu "Mbili" akawarudisha kwenye sinia akisema "Wazee wangu nadhani japo shule hamkwenda ila mnajua moja+mbili=tatu(1+2=3) hivyo tunao Kuku watatu mezani"
Baba akiwa na tabasamu pana akasema
"Mmh! Kweli mwanangu umesoma
SASA TUFANYE HIVI
MIMI NACHUKUA KUKU MMOJA NA MAMA YAKO WA PILI WEWE UTAKULA HUYO WA TATU ULIYESEMA"
Zephiline hakutegemea
Alibaki amewatolea macho wazazi wake wakila Kuku mbele ya macho yake
Jamani tupunguzeni ujuajiπ€£ #ChekanaZephiline
Chapisha Maoni