Pesa Sio Utajiri 🤔
Walifikia kwa mkulima mmoja na kukaa siku kadhaa
Siku ya kuondoka walipokua njiani Baba alimuuliza mtoto wake "Umejifunza nini katika maisha ya wanakijiji?"
Mtoto akajibu "Sisi tuna Mbwa mmoja wao wanao wengi
Tuna swimming pool wao wana mito
Tunawasha taa usiku wao wana nyota
Tuna nunua chakula wao wanatengeneza cha kwao
Nyumba yetu imezungukwa na ukuta wao wana marafiki
Tuna televisheni wao wanatumia muda wao kukaa na marafiki familia na wageni mfano sisi"
Baba akakosa neno la kusema kisha mtoto akamaliza kwa kwa kusema "Ahsante Baba kwa kunionesha jinsi gani tulivyo maskini"
JIFUNZE
Sio pesa ndio inafanya mtu awe tajiri bali ni:
Upendo
Utu wema
Mahusiano mazuri
Marafiki na Amani
Ndio humfanya mtu kuwa tajiri🙏🏽 #ChekanaZephiline
Chapisha Maoni