'Nakuzidi Utundu' π
Dada: Ninaweza kupika zaidi yako
Mama: Nani kakwambia?
Dada: Kaniambia mume wako
Mama: Sababu ya pili?
Dada: Ninaweza kupiga pasi na kunyoosha nguo zaidi yako
Mama: Nani kakuambia?
Dada: Mume wako
Mama: Eeh kumbe huyu ndio anakupa kichwa cha kuwa na jeuri hizo ngoja arudi hapa anione
Nataka kukuambia kuwa mimi ndio mmiliki wa hii nyumba kama sijaamua mimi jambo la humu ndani yeye sio lolote hata uwe unaibeba hii nyumba na sisi tumo ndani tumelala hauwezi kuongezewa mshahara hapa
Hebu nitokee hapa na uso wake na kama unaanza tabia zako za ajabu kesho nakukatia tiketi urudi kijijini kwenu maana unataka kuota mbawa
Kipi kingine ulichonizidi hebu niambie?
Dada: Nakuzidi kwa utundu kitandani
Mama: Pumbaaaavu na hivyo mlifanya huo upuuzi wenu na mpaka akaamua kukusifia si ndio?
Dada: Hapana sio yeye aliyenisifia hivyo
Mama: Ni nani aliyekusifia huo upuuzi wako?
Dada: Ni dereva wako ndiye aliniambia nimekuzidi kwa utundu kitandani
Mama: Oooooh! punguza sauti mwanangu nakuongezea mshahara tena mara mbili nilikuwa nakujaribu tu sawa Mama?
π€£π #ChekanaZephiline
Chapisha Maoni