Sasa tuendelee kwa kumuona Bakari akiwa na furaha kwani Shilingi ile ilikuwa na thamani kubwa sana
Mdogo wake anakuwa mtu wa mambo mengi hivyo anamzuia Kaka yake kwenda kupeleka Shilingi sehemu husika ili apate pesa
Shilingi inaanza kuwatesa Bakari na mdogo wake baada ya binti kutekwa akitakiwa kusaidia upatikanaji wa Bakari
Anateswa mpaka anataja namba ya Kaka yake ambapo wanampigia na kumwambia alete Shilingi ili apewe ndugu yake
Bakari katika harakati zake anakutana na yule dada chizi aliyempa ile Shilingi
Kwa mawazo ya haraka anahisi yule dada anahusika na mikasa yote anayoipitia Bakari akiwa na ile Shilingi
Wanakimbizana sana mpaka Bakari anapochoka huku chizi akimcheka tu
Lengo la Bakari linabadilika baada ya kugundua kweli bado dada ni chizi hivyo anamuuliza kuhusu Shilingi japo hapati majibu sahihi ya maswali anayomuuliza yule chizi
Anapokea simu ambayo inamtaka aelekee alipo ndugu yake
Inambidi anawahi ili kutatua matatizo yanayomkuta ndugu yake
Cha kushangaza sasa ambachokutana nacho Bakari kinamfanya anashangaa tu
Hiki kitu naomba Play filamu utajionea mwenyewe
Bwana wee
Bakari anaiacha Shilingi na kumchukua ndugu yake na maisha yanaendelea
Siku chache baadae anakuja yule jambazi tena katika kijiwe anachofanyia kazi na kinachotokea hapo kitakushangaza sana