Kizazi cha Dawa | Ep 02

Tuliishia Simon na mkewe walipokutana na mauza uza ya chakula kugeuka mchanga hivyo tuendelee na mkasa wetu

Baada ya hapo tutakutana na Simon akishangaa kumuona mdada mbele aliyejitambulisha kuwa ni binti yake Neema wakati Simon anajua mwanae ni mdogo na amelala ndani

Simon alienda kwa washikaji zake na cha ajabu alikuwa mkali kwao bila sababu za msingi lakini waligundua hilo na wakaahidi kumsaidia

Mke wa Simon akiwa nyumbani amejipumzisha aliota ndoto ambayo anaonekana yule dada aliyemtokea Simon na kusema ni mwanae Neema
Marafiki zake Simon walifika mpaka nyumbani na kumkuta shemeji yao ambaye baada ya kumuita alistuka na waliishia kumuulizia rafiki yao Simon na wakaondoka

Mauza uza yanaendelea baada ya Simon na mkewe usiku wakiwa wamelala huku Simon akiwaacha mke wake na mwanane chumba tofauti
Kumbe yule Neema alikuwa ni jini ambaye ndio yule mganga waliyeenda kumuomba mtoto naye alimpenda Simon hivyo kujiingiza katika uzao wao ili ampate Simon

Simon akiwa amelala ndipo yule jini akaenda kufanya naye mapenzi bila Simon na mke wake kujua chochote

Simon baada ya kuona mambo hayaeleweki akaenda kwa mzee ambaye aliona kwa umri wake angemsaidia kumshauri au kujua jinsi gani anaweza kutatua changamoto za familia yake ambapo mzee yule alimshauri Simon aende kwa waganga ili kutafuta ufumbuzi wa jambo lile

Simon alichukuliwa na yule rafiki yake na kwenda kwa mganga ambaye aliahidi kumsaudi

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Fomu ya Anwani