Maisha yalikuwa magumu sana kwa Mariam ambaye amesoma na hakupata kazi hivyo akatakiwa kubaki kijiji kwa Bibi yake huku akisubiri siku Mungu amjaalie apate kazi yeyote ile yenye kukidhi mahitaji yake
Mungu humpa mtu muda wake ukifika na ukiwa mvumilivu
Siku moja Mariam akiwa shambani analima akapigiwa simu ya kupewa kazi hivyo ikamlazimu kwenda mjini kuanza kazi
Philipo ni kijana ambaye alikuwa na maisha yake kabla lakini yaliharibika kwa sababu ya mahusiano
Alishawahi kufungwa jela na sasa yupo uraiani akiwa kaamua kuyaanza upya maisha yake
Philipo na Mariam wanakutana katika mazingira ya kazi ambako Philipo alikuwa akiuza mkaa
Mariam anatokea kumpenda Philipo ghafla wanapoonana siku hiyo hiyo ya kwanza kukutana
Katika kazi za Philipo kuna majaribu mengi sana yanatokea hivyo Philipo huishia kuyakabili na kuyatatua
Siku hii Philipo anaenda ofisini kwa Mariam ambapo kumbe huwa anajihusisha na kazi nyingine nje ya ile ya kijiwe cha kuuza mkaa
Ajabu na bila yeye kujua anakutana na Mariam pale ofisini na Mariam anatumia fursa ile kumpa Philipo
Unahisi nini kiliendelea hapo na je ungependa kuyaona maisha haya katika video?
Basi play video hii ujionee