Shilingi | Ep 02

Baada ya kumuona Bakari akijiachisha kula na kumsaida chizi aliyemuomba chakula na akapewa Shilingi basi tuendelee na mkasa wetu

Kama tulivyoona Bakari alikuwa na mpenzi msaliti, sasa katika muendelezo huu tutamuona akija na jamaa yake na kumdhihaki sana Bakari
Ni mengi sana yatatokea hapa mpaka kumfanya Bakari alie kilio kama mtoto baada ya mpenzi wake huyo kumdhihaki vya kutosha

Bakari anaenda sehemu na kukaa zake kupunguza msongo wa mawazo ndipo anaona gazeti lenye habari zinazomfanya ashangae sana
Zinahusu ile Shilingi aliyopewa na Chizi pale mgahawani

Kuna mengi yanaendelea lakini naomba tukomae na Bakari kwanza
Bakari anapopata zile habari gazetini anajipa kazi ya kumtafuta yule chizi na hampati

Bakari ana ndugu yake anasoma chuo na yeye ndio anahitajika kumsaidia kama Kaka mkubwa
Kwa maisha yale tulioona kwenye mkasa uliopita unahisi anawezaje?
Basi ndugu yake huyo anafukuzwa chuo kwa kushindwa kulipa gharama za masomo

Haya na mengine yote yatazame katika filamu hii

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Fomu ya Anwani