Baada ya kuona dada mdogo wa Sofia alivyochukizwa na kitendo cha dada yake kuacha watoto na kwenda kulala nyumba za wageni na Lava basi tuendelee na filamu yetu hii nzuri yenye mafunzo ndani yake
Combo aliachwa na askari akiahidi kuacha zile tabia chafu za kusambaza pesa mbandia lakini hakuacha
Leo alifumaniwa tena akimtuma dada yake kwenda kwa wakala kuweka pesa bandia na akamkamata
Dada yake Combo alimwambia Mama yake na Mama Combo akafuatilia kesi hiyo
Mussa pia alikuwa amekamatwa hivyo leo aliambiwa aseme ukweli wa anayemtuma au kufanya naye kazi ndipo awe huru
Mussa alimkutanisha askari na Boss wake na ndipo alipokamatwa na Mussa kubaki huru huku Mama yake Combo pia akiambiwa hata Combo atakuwa huru