Combo amekuwa mtu wa kuhangaika huku na kule akifanya hiki na kile ili tu apate pesa za kuisaidia familia yake yaani dada yake mdogo na Mama yake
Combo anakubali kufanya kazi yeyote ili hata ngumu kiasi gani ili tu apate pesa za kumkimu katika mahitaji yake
Kwa upande wa Lava maisha yake sio mabaya, anaishi kwa furaha yeye na familia yake
Combo anapata kazi ya saluni akijua ni halali kumbe mwenye saluni ana mishe zake za siri ambazo anazifanya na kujifichia kwenye unyoaji
Combo na Lava wakiwa na Mussa mmliki wa Saluni wanakutana na kuongea mawili matatu kisha Lava na Mussa wanamuacha Combo na kwenda ofisini kwa Mussa
Combo hakuwa kabisa mzoefu wa kazi za saluni sasa kuna mteja anakuja kunyolewa na Combo anajikuta anakosea kumnyoa mteja yule😂
Naomba nisikwambie mengi naomba tazama filamu hii ili ujionee mwenyewe mwanzo mwisho