Penzi la Usaliti | EP 03

Tuliishia pale ambapo Philipo aliambiwa amechaguliwa katika kampuni ile aliyoomba kazi hivyo tutaona yanayofuata katika muendelezo huu
Philipo alipata kazi na akaelekezwa utendaji wa kazi unavyoenda

Maisha yaliendelea huku maisha ya Philipo na mkewe Mariam yakiwa ya kuvutia na ya furaha
Walienda sokoni pamoja, walifanya mazoezi pamoja na mengine mengi

Philipo alikuwa na wazo kuhusu maisha yao ya mbele hivyo alimshirikisha mkewe ili wafikiri ni jambo gani la kufanya kwakuwa ajira huwa zina changamoto mbalimbali inaweza tokea siku hawana kazi na hawana pakuanzia hivyo wajue watasaidiwa na nini

Miezi kadhaa ilipita
Philipo alibadilika na kuwa na tabia zisizoeleweka kabisa
Mke wake hakumchoka ila alihisi angeweza kumbadili muda ukifika lakini mambo yakazidi kuwa mabaya zaidi

Usiku mmoja mke wa Philipo alipokea simu ya mumewe kwakuwa iliita huku Philipo akiwa na usingizi mzito
Kumbe ile simu haikuwa nzuri kabisa kwake Mariam kwakuwa ilimfanya aliye sana usiku ule na hata Philipo alipoamka na kukuta mkewe akilia alidanganywa sababu ni Bibi kule kijijini anaumwa sana

Usiku ule ulipita
Kumbe Mariam aliamua kufanya uchunguzi kwa siri sana na ndipo alikutana na tukio ambalo hakuwahi kulitegemea katika maisha yake
Unahisi ni nini hicho, tazama filamu hii ujionee matukio yote ndani yake


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Fomu ya Anwani