Bakari ni muhitimu wa chuo ambaye licha ya kutafuta kazi kwa juhudi zote bila kukata tamaa anaikosa kazi
Mke wa Bakari anabeba mimba ambayo anadai ni ya mchepuko wake
Maisha ya Bakari ni ya shida kiasi cha kukosa pesa ya kula kabisa
Bakari ana rafiki yake muuza duka hivyo anatumia urafiki ule kupata msaada wa chakula lakini rafiki yake anamwambia hana pesa hivyo ingependeza kama angefanya shughuli ili impatie pesa ya kula
Bakari anaenda sehemu na kukaa zake kupunguza msongo wa mawazo ndipo anaona gazeti lenye habari zinazomfanya ashangae sana
Zinahusu ile Shilingi aliyopewa na Chizi pale mgahawani alipoenda kula akakutana naye na kumpa chakula chake kisha chizi akampa hiyo Shilingi ambayo kumbe ina thamani kubwa sana
Bakari ana ndugu yake anasoma chuo na yeye ndio anahitajika kumsaidia kama Kaka mkubwa
Mdogo wake anakuwa mtu wa mambo mengi hivyo anamzuia Kaka yake kwenda kupeleka Shilingi sehemu husika ili apate pesa
Shilingi inaanza kuwatesa Bakari na mdogo wake baada ya binti kutekwa akitakiwa kusaidia upatikanaji wa Bakari