Simon alikuwa na mke wake ambaye licha ya maisha magumu sana lakini walipendana sana lakini walikuwa na tatizo la kutokuwa na mtoto
Simon na mkewe walikuwa na tamaa sana ya kuwa na mtoto lakini hawakujaaliwa kabisa kumpata
Leo waliwaza jinsi gani wapate mtoto na mawazo makuu ikawa ni kwenda kwa mtaalamu ili wakapewe tiba na suluhisho la kupata mtoto
Hii Simon alifanya bila kumshirikisha mkewe moja kwa moja japo naye baada ya kugundua hakuwa na kipingamizi chochote
Walifika kwa mganga na kuelezea shida zao na mganga akaahidi kuwasaidia huku akiwapa masharti na wakakubali kuwa wangeweza kuyatimiza
Upande mwingine tutakutana na majini yakicheka kwa furaha na kuonesha kuna jambo zuri kwao limetokea na cha kushangaza ni yule mganga ni miongoni mwao na ndiye alikuwa akishangiliwa kwa ujio wake duniani
Baada ya kutoka kwa mganga mke wa Simon alinasa ujauzito na dalili za mwanzo zikaonesha
Baada ya kipindi fulani muda ulifika wa mke wa Simon kujifungua na akajifungua mtoto salama
Maisha yaliendelea kama kawaida na bila kujua chochote Simon alikutana na viatu ambavyo ndani ya filamu utaona aliyeviacha hivyo akavichukua kwani hakuona nani ameviacha pale
Simon alikuwa akijishughulisha na kilimo hivyo alikuwa anapambana kulima mashamba ya watu ili ajipatie kipato hivyo alifanya hivyo ili apate pesa za kulisha familia yake