Penzi la Usaliti | EP 04

Tuliishia pale ambapo Mariam alimfumania mume wake akielekea nyumba za kulala wageni akiwa na binti mwingine

Maamuzi makubwa aliyoyachukua Mariam ilikuwa ni kwenda kazini kwa Philipo na kutoa malalamiko yake na cha ajabu kumbe hata vile vyeti vilikuwa vya kugushi na aliyefanya hayo yote alikuwa ni Mariam mwenyewe kwa ajili ya kumsadia mumewe

Philipo alipofika tu kazini aliitwa na maagizo ilikuwa ni kuhusu kuachishwa kazi hivyo aliikosa kazi kwa sababu ya mkewe kumsemea makosa na mbaya zaidi ni suala la vyeti

Philipo alirudi nyumbani huku akiwa na hasira kwa kitendo alichokifanya mkewe kule kazini hivyo mengi yalitokea wakiwa ndani baada ya kukutana

Baada ya yaliyojili usiku ule
Philipo aliamua kwenda kwa mjomba wake kwenda kushitaki kuhusu jambo lile

Mjomba alipopata taarifa zile alimhakikishia Philipo kurudi kazini na mambo mengine yatakuwa sawa

Baada ya pale mjomba alienda kwake Philipo kwa ajili ya kuonana na mke wa mwanae ili kujua nini kinaendelea
Kwa kufupisha stori hii, mjomba alipofika na kupata uhakika aliahidi mambo magumu sana ambayo yalimfanya mke wa mwanae yaani Mariam kupata wasiwasi na alipokutana na rafiki zake alipewa wazo la kwenda kwa mganga ili kuweka mambo yale sawa

Basi naomba tazama tukio zima ili uone nini kiliendelea kwa mganga na nini kilichofuata baada ya hayo yote


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Fomu ya Anwani